Esoma-KE Logo
Change Class  |  Change Subject

Ngeli za Kiswahili - Class 8 Kiswahili

Ngeli za Kiswahili

  Change Class CLASS 8
Select Subject  |  Kiswahili
  Change Topic

Guest Account

Hello Guest, Create an Account or Login to save your progress and get unlimited access to more notes, revision exercises and answers.

Feeling Ready?

Attempt Class 8 Kiswahili Questions

Guest Account
Hello guest, kindly login to access unlimited study notes and revision questions.

Create an account / login to help track your progress and unlock more features including additional notes, rapid quizzes, revision questions, virtual library, and the new Esoma Classroom

Ngeli za Kiswahili

Last Updated: 14th April, 2021

- Ngeli ni vikudi vya majina ambavyo, kwa mfumo wa kisasa na unaokubalika, huundwa kwa kuunganisha viambishi viwakilishi vya nomino
mfano 1:
"Kijiko kimepotea" kwa wingi ni "Vijiko vimepotea"
- Kwa kuunganisha viambishi KI na VI tunapata ngeli ya KI-VI. Ni vyema kuelewa kuwa tumezingatia viambishi wala si sarufi.
mfano 2:
"Mti umeanguka - Miti imeanguka". Ngeli inayoundwa ni ngeli ya U-I

Aina za Ngeli

A-WA

Ngeli hii huchukua nomino na viumbe wenye uhai. Kama vile binadamu, wanyama na kadhalika. Kwa mfano; mtu-watu, Ng'ombe-Ng'ombe, Mkunga-Wakunga.
Mifano katika sentensi
a) Mtu huyu ametoka sokoni - Watu hawa wametoka sokoni
b) Nyuki huyu atatengeneza asali - Nyuki hawa watatengeneza asali

KI - VI

Ni ngeli ya majina:
- ya vitu visivyo hai
- yanayoanza kwa kiambishi KI au CH kwa hali ya umoja na kiambishi VI au VY kwa hali ya wingi
- ya vitu vingine katika hali ya udogo
Mifano katika sentensi
a) Kiatu changu kimepakwa rangi - Viatu vyangu vimepakwa rangi
b) Choo hiki kimeoshwa sasa hivi - Vyoo hivi vimeoshwa sasa hivi
c) Kitoto hiki kinalia ovyo - Vitoto hivi vinalia ovyo

LI - YA

Hii ngeli huundwa na majina yanayoanza kwa kiambishi LI katika hali ya umoja na kwa kiambishi YA katika hali ya wingi. Pia, maneno yaliyo katika hali ya ukubwa huchukua ngeli ya LI - YA
Baadhi ya majina haya huchukua muundo wa JI - MA (Jiwe - Mawe).
Mifano katika sentensi
a) Ngunia limeraruka - Magunia yameraruka
b) Dawati limevunjika - Madawati yamevunjika
c) Jitu limekalia kiti - Majitu yamekalia viti

U - I

Hujumuisha majina yaanzayo kwa sauti M katika hali ya umoja na sauti MI katika hali ya wingi
Ngeli hii huchukua kiambishi ngeli U katika hali ya umoja na kiambishi ngeli I katika hali ya wingi
Mifano katika sentensi
a) Mswaki wake ulipotea - Miswaki yao ilipotea
b) Mti ule uko na tunda - Miti ile iko na tunda
c) Mwembe huu ni wangu - Miembe hii ni yetu

I - ZI

Hutumiwa kwa majina yasiyobadilika kwa umoja wala kwa wingi lakini huchukua viambishi viwakilishi tofauti: I katika hali ya umoja na ZI katika hali ya Wingi
Mengi yake huanza kwa sauti /u/, /ng/, /ny/, /mb/, na kadhalika
Mifano katika sentensi
a) Nyumba yetu imeoshwa - Nyumba zetu zimeoshwa
b) Dawa ya kulevya ni hatari - Dawa za kulevya ni hatari
c) Ndizi hii ni tamu - Ndizi hizi ni tamu

YA - YA

Ngeli hii hujumuisha majina ya vitu visivyoweza kuhesabika (nomino za wingi).
Hayana umoja. Mengi ya majina haya huanza kwa MA lakini yanaweza kuchukua muundo wowote.
Mfano katika sentensi
a) Maji yote yamemwagika - Maji yote yamemwagika

U - ZI

Hii ngeli hutumiwa kwa majina ambayo huanza kwa U katika hali ya umoja na ZI katika hali ya wingi.
Majina yenye silabi tatu au zaidi hubadilishwa kwa wingi kwa kutoa sauti /u/ kama vile Ufunguo-Funguo. Majina ya silabi mbili huongezewa /ny/ katika wingi. kama vile Uso - Nyuso.
Mifano katika sentensi
a) Uso wake uko na alama - Nyuso zao ziko na alama
b) Ulimi wake unauma - Ndimi zao zinauma
c) Ufunguo wangu umepatikana - Funguo zetu zimepatikana

U - U

Hii ngeli hujumuisha majina:
- ya vitu visivyo gawika wala kuhesabika
- ya kufikiria tu
- ya nomino za wingi yanaoanza kwa sauti /u/ au /m/
Majina haya hayana wingi
Mifano katika sentensi
a) Unga umemwagika - Unga umemwagika
b) Ujanja huu ni mbaya - Ujanja huu ni mbaya

PA - KU - MU

PA ni ngeli ya mahali/pahali maalum na panapodhihirika
KU ni ngeli ya mahali jumla na ambayo si dhahiri
MU ni ngeli ya mahali ndani
Mifano katika sentensi
a) Mahali hapo ni safi - Mahali hapo ni safi
b) Huku ni kwa dada yangu - Huku ni kwa dada yangu
c) Humu mna giza - Humu mna giza

Hello Guest, Please help review these notes.    Why review

Your review has been successfully submitted.
Tell us what you think about the notes.

Submit Comment