Esoma-KE Logo
Change Class  |  Change Subject

Alama za Kuakifisha - Class 7 Kiswahili

Alama za Kuakifisha

  Change Class CLASS 7
Select Subject  |  Kiswahili

Guest Account

Hello Guest, Create an Account or Login to save your progress and get unlimited access to more notes, revision exercises and answers.

Feeling Ready?

Attempt Class 7 Kiswahili Questions
Guest Account
Hello Guest, Create an Account or Login to save your progress and get unlimited access to more notes, revision exercises and answers.
Hello guest, these notes have a free access. Enjoy.

Create an account / login to help track your progress and unlock more features including additional notes, rapid quizzes, revision questions, virtual library, and the new Esoma Classroom

Alama za Kuakifisha

Kikomo au nukta (.)

Huonyesha sentesi imekamilika.
Mfano
Mamake ameenda sokoni.

Kiulizi (?)

Hutumika kuuliza swali.
Mfano
Ni mpira upi uliochezewa na watoto asubuhi?

Alama ya kipumuo / koma / Kituo (,)

Hutumika kwa njia zifuatazo

a) Kugawanya sentensi ndefu na kumpa msomaji nafasi ya kupumua

Mfano
Tuliposafiri kwa saa nane, tulipumzika kidogo kisha tukaendelea na safari yetu.

b) Kuorodhesha mambo au vitu

Mfano
Tumeenda sokoni kununua nyanya, vitunguu, mboga na dania za kupikia wageni.

c) Kutoa maelezo zaidi kuhusu jambo au kitu

Mfano
Bwana Kazungu, mwalimu mkuu wa shule yetu, ndiye mkuu wa Kiswahili.

Herufi kubwa

Herufi kubwa hutumika mwanzoni mwa sentensi, mwanzoni mwa jina la mtu au mji, nchi au mahali.
Mfano
Mto Tana na Athi ndiyo mito mirefu zaidi nchini Kenya.

Kihisishi / mshangao / kimako (!)

Hutumika kuonyesha hisia tofauti kama vile; furaha, mshangao, hasira au huzuni.
Mfano
Lo! unamshika nyoka.
Huree! tumeushinda uchaguzi kwa awamu nyingine.

Vidondozi / vinukuu / vinukulu (")

Hutumika kwa njia zifuatazo:

a) Hutumiwa kuonyesha usemi halisi au maneno yalivyosemwa bila kuyabadilisha

Mfano
"Endeni mchezee uwanjani," mwalimu aliwaeleza watoto.

b) Kuonyesha neno lisilo la kiswahili.

Mfano
Watu wanapopika "chips" hutumia mafuta.

Mkwanju / Mkato (/)

Hutumika kuorodhesha mambo au maneno yenye maana sawa.
Mfano
Magari ya matwana / matatu / daladala hutumika zaidi nchini kenya.

Dukuduku / vitone (...)

Huonyesha kuwa usemi haujakamilika ama kuna maneno ambayo hayajaandikwa.
Mfano
Sitasema jambo lolote lakini ...

Koloni / nukta mbili (:)

Hutumika kwa njia zifuatazo:

a) Hutumiwa kuonyesha usemi halisi au maneno yalivyosemwa bila kuyabadilisha

Mfano
Viungo vya mapishi vilivyo nunuliwa na mama vilikuwa: dania, masala, tangawizi na karafuu.

b) Katika uandishi wa mazungumzo

Mfano
Mwalimu: Mbona umechelewa kuingia darasani?
Koki: Samahani mwalimu, gari la kubebea wanafunzi limechelewa leo.

Nusu koloni / nukta mkato (;)

Hutumika kuonyesha sehemu ya pili inayoelezea zaidi kuhusu sehemu iliyotangulia.
Mfano
Alionywa kwa kosa hili mara tatu; hajabadilika hata kidogo.

King'ong'o / ritifaa (')

Hutumika kukata neno ilikubadilisha sauti.
Mfano
Ng'ombe huyu hula zaidi kila siku.

Mabano / Parandesi( )

Hutumiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu jambo liIilosemwa
Mfano
Ezekiel Kemboi (mwanariadha mashuhuri) ameishindia Kenya dhahabu katika mashindano mablimbali duniani.

Kistari kifupi (-)

Hutumika kwa njia zifuatazo:

a) Kusisitiza sauti

Mfano
Walmcheka ha-ha-ha alipoingia darasani.

b) Kuunganisha tarakimu kuonyesha mwanzo hadi mwisho

Mfano
Alikuwa naibu mwalimu mkuu kutoka 2013-2017.

Hello Guest, Please help review these notes.    Why review

Your review has been successfully submitted.
Tell us what you think about the notes.

Submit Comment