- Hutegemea nyakati tofauti, umri wa waamkianao na mafungamano kati ya wanaoamkiana.
- Kinyume cha maamkizi ni maagano yaani, maneno wanayoambiana watu wanapoagana.
Maamkizi au Maagano | Jibu | Wakati |
---|---|---|
Hujambo? | Sijambo | Wowote |
Shikamoo? | Marahaba | Wowote |
Sabalkheri? | Alheri | Asubuhi |
Masalkheri? | Alheri | Jioni |
Chewa | Chewa | Asubuhi |
Buriani | Buriani dawa | Wowote |
Alamsiki | Binuru | Usiku |
Kwaheri ya kuonana | Mungu akipenda | Wowote |
Waambaje? | Sina la kuamba | Wowote |
Lala unono | Nawe pia | Usiku |
Adabu/staha | Wakati |
---|---|
Samahani, kumradhi na kunradhi | Hutumika kuomba radhi au kumtafadhalisha mtu akupishe au akusikilize. |
Simile, habedari! na heria! | Hutumika na mtu anayeomba nafasi apite au kutahadharisha. |
Tafadhali | Hutumika kumsihi mtu atende jambo kwa fadhila zake. |
Mstahiki | Ni neno linalotangulia jina la mtu mwenye mamlaka na aliye na haki ya kuheshimiwa. |
Marehemu au hayati | Ni jina linalotajwa kabla ya jina la mtu aliyefariki na aliyekuwa mwadilifu. |
Muadhama, mwadhamu au muhtaramu | Ni jina la heshima aitwalo mheshimiwa |
Siti | Ni jina la heshima lamwanamke linalotangulia kabla ya jina lake hasa |
Kutabawali | Ni neno la heshima linalomaanisha kwenda haja ndogo, kukojoa. |