- Hutegemea nyakati tofauti, umri wa waamkianao na mafungamano kati ya wanaoamkiana.
- Kinyume cha maamkizi ni maagano yaani, maneno wanayoambiana watu wanapoagana.
| Maamkizi au Maagano | Jibu | Wakati |
|---|---|---|
| Hujambo? | Sijambo | Wowote |
| Shikamoo? | Marahaba | Wowote |
| Sabalkheri? | Alheri | Asubuhi |
| Masalkheri? | Alheri | Jioni |
| Chewa | Chewa | Asubuhi |
| Buriani | Buriani dawa | Wowote |
| Alamsiki | Binuru | Usiku |
| Kwaheri ya kuonana | Mungu akipenda | Wowote |
| Waambaje? | Sina la kuamba | Wowote |
| Lala unono | Nawe pia | Usiku |
| Adabu/staha | Wakati |
|---|---|
| Samahani, kumradhi na kunradhi | Hutumika kuomba radhi au kumtafadhalisha mtu akupishe au akusikilize. |
| Simile, habedari! na heria! | Hutumika na mtu anayeomba nafasi apite au kutahadharisha. |
| Tafadhali | Hutumika kumsihi mtu atende jambo kwa fadhila zake. |
| Mstahiki | Ni neno linalotangulia jina la mtu mwenye mamlaka na aliye na haki ya kuheshimiwa. |
| Marehemu au hayati | Ni jina linalotajwa kabla ya jina la mtu aliyefariki na aliyekuwa mwadilifu. |
| Muadhama, mwadhamu au muhtaramu | Ni jina la heshima aitwalo mheshimiwa |
| Siti | Ni jina la heshima lamwanamke linalotangulia kabla ya jina lake hasa |
| Kutabawali | Ni neno la heshima linalomaanisha kwenda haja ndogo, kukojoa. |
