Create an account / login to help track your progress and unlock more features including additional notes, rapid quizzes, revision questions, virtual library, and the new Esoma Classroom
Matumizi ya Vivumishi vya Pekee Enye na Enyewe Pamoja na Ngeli
'Enye' - Huonyesha umilikaji.
- Enye hufuatwa na nomino (kama vile: Mwalimu mwenye gari)
'Enyewe' - Huonyesha kinachohusika (au anaye husika).
Mifano
Ngeli |
Enye |
Enyewe |
|
(Enye) Umoja |
(Enye) Wingi |
(Enyewe) Umoja |
(Enyewe) Wingi |
A-WA |
mwenye |
wenye |
mwenyewe |
wenyewe |
KI-VI |
chenye |
vyenye |
chenyewe |
vyenyewe |
U-I |
wenye |
yenye |
wenyewe |
yenyewe |
LI-YA |
lenye |
yenye |
lenyewe |
yenyewe |
U-ZI |
wenye |
zenye |
wenyewe |
zenyewe |
I-ZI |
yenye |
zenye |
yenyewe |
zenyewe |
U-U |
wenye |
wenye |
wenyewe |
wenyewe |
Mifano Katika Sentensi
1a. Mwalimu mwenye ujuzi ni huyu.
1b. Mwalimu mwenyewe ana ujuzi.
2a. Nyimbo zenye utamu zimeimbwa kanisani.
2b. Nyimbo zenyewe zinautamu.
3a. Jicho lenye kasoro linauma.
3b. Macho yenyewe yana kasoro.
4a. Kitabu chenye kurasa nyingi kimepotea.
4b. Vitabu vyenyewe vina kurasa nyingi.
Tahadhari
- Enye halifuatwi na Kitenzi. Kama vile: Mwalimu mwenye anafunza ana ujuzi. Hio mfano sio sahihi.
Hello Guest, Please help review these notes. Why review
Your review has been successfully submitted.
Tell us what you think about the notes.
We are sorry for this interruption.
Please create a MEMBERSHIP Account to continue reading
Why am I seeing this?
DISMISS MESSAGE