Maamkizi - ni kujulia mwenzako hali (kumsabahi).
Salamu - Taarifa ya maamkizi inayotolewa na mtu, moja kwa moja au kupitia mtu mwingine.
- Maamkizi ni sawa na salamu
| Salamu | Jibu |
|---|---|
Salamu Za Asubuhi |
|
| Habari Za Asubuhi | Njema / Nzuri |
| Chewa | Chewa |
| Sabalkheri | Aheri / Sabalkheri |
Salamu Za Mchana |
|
| Habari Za Mchana | Njema / Nzuri |
| Umeshindaje | Vyema / Salama |
Salamu Za Jioni |
|
| Masalkheri | Aheri / Masalkheri |
| Habari Za Jioni | Njema / Nzuri |
Kuagana Usiku |
|
| Alamsiki | Binuru |
| Lala Salama | Wasalimini |
| Ndoto Njema | Ya Mafanikio |
Salamu Nyinginezo |
|
| Salaam Aleikum | Aleikum Salaam |
| Buriani | Buriani dawa |
| Shikamoo | Marahaba |
| Pole | Nishapoa |
| Tuonane Kesho | Inshallah / Mungu akipenda |